WATENDAJI 7 WA SERIKALI WASIMAMISHWA KAZI KWA UPOTEVU WA MIL 900 | BONGOJAMII

WATENDAJI 7 WA SERIKALI WASIMAMISHWA KAZI KWA UPOTEVU WA MIL 900

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imewasimamisha kazi watendaji waandamizi na wakuu wa idara saba wa manispaa hiyo kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha ya halamshauri hiyo ya Sh milioni 900.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava alisema kuwa maamuzi hayo yamefanyika kupitia kikao cha fedha na uongozi cha halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Kigoma.

Meya Ruhava alisema kuwa maamuzi hayo ya kamati ya fedha na uongozi yametokana na taarifa ya mkaguzi wa ndani inayoonesha kuwepo kwa matumizi yanayotia shaka ya kiasi cha zaidi ya Sh milioni 900 ambazo maelezo yake na vielelezo vilivyopo vinatia shaka.

Pamoja na hilo ametoa agizo kukamatwa na kuhojiwa kwa baadhi ya watalaamu kwa madai ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha isivyo halali.

Aliwataja waliosimamishwa kuwa ni pamoja na mhandisi wa ujenzi Boniface William, mhandisi msaidizi wa ujenzi, Wilfred Shimba na mkuu wa kitengo cha manunuzi, Baruti Baruti.

Aidha, katika orodha hiyo wapo wataalamu ambao ama wamefukuzwa kazi, kusimamishwa na wengine kuhamishwa ambapo watatakiwa kuhojiwa na Polisi na pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, kughushi nyaraka na kujipatia fedha kinyume na utaratibu wa sheria za fedha za halmashauri hiyo.

Wanaotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Boniface Nyambele na aliyekuwa mhandisi wa maji, Sultan Ndoliwa ambao wamehamishiwa halmashauri nyingine nje ya mkoa Kigoma, Dokta John Chacha Maginga ambaye ameacha kazi, mweka hazina wa Halmashauri hiyo, Marco Michale ambaye amesimamishwa na Christina Nyumaihunzi ambaye alifukuzwa kazi mwishoni mwa mwaka jana.

Alisema kuwa pamoja na baadhi ya watuhumiwa hao kuhamishwa, kufukuzwa au kusimamishwa kazi watatakiwa kuja kujibu tuhuma hizi za sasa zinazowakabili na kwamba tayari maelekezo yameshatolewa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia watuhumiwa hao.

Katika hatua nyingine, Meya Ruhava ameomba kufanyika kwa ukaguzi maalumu wa fedha na miradi ili kubaini usahihi wa matumizi ya fedha zilizoelekezwa katika matumizi mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ili kuona usahihi wa tuhuma zao na kuweka sawa mapato na matumizi ya halmashauri.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts