ASILIMIA YA WENYE VYETI FEKI UDSM YAWEKWA HADHARANI | BONGOJAMII

ASILIMIA YA WENYE VYETI FEKI UDSM YAWEKWA HADHARANI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

WAKATI fagio dhidi ya watumishi wenye vyeti vya kughushi vya kielimu na taaluma likiacha mtikisiko kwa baadhi ya taasisi za serikali-


Imebainika kuwa operesheni hiyo haijaathiri mwenendo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya watumishi 24 tu kukumbwa na kadhia hiyo kati ya 1,664 waliohakikiwa, sawa na asilimia 1.4 tu.


Aidha, katika uhakiki huo uliohusisha watumishi wote wa taasisi za umma nchini, ni watumishi 128 tu wa UDSM ndiyo waliokutwa wakiwa na taarifa zisizokamilika kuhusiana na vyeti vyao.


Makamu Mkuu wa UDSM, Prof. Rwekaza Mukandala, aliiambia Nipashe kuwa tangu ukaguzi ulipoanza katika chuo hicho mwaka jana, watumishi 24 walikutwa na vyeti vya kugushi.


Alisema katika operesheni hiyo mtumishi mmoja alikutwa na cheti chenye utata, huku watumishi 128 waliwasilisha vyeti ambavyo havikutimia.


Alisema katika kazi hiyo, watumishi 1,511 wa UDSM waliwasilisha vyeti kamilifu na halali kwa ajili ya ukaguzi.


“Wafanyakazi 24 waliokutwa na vyeti vya kugushi hawajafukuzwa kazi na kwa sasa mchakato wa kuchukuliwa hatua stahiki unaendelea,” alisema Profesa Mukandala.


Profesa Mukandala alisema watumishi waliokutwa na vyeti vya kugushi wengi wao wanatoka idara ya polisi, udereva, mapokezi na watumishi wa kada za chini.


Kazi ya uhakiki wa vyeti vya elimu na taaluma kwa watumishi wote wa umma ilianza Machi, mwaka jana, lengo likiwa kuongeza ufanisi katika kuwatumikia Watanzania na kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania wenye sifa kitaaluma.


Tangu kuanza kwa kazi hiyo, zaidi ya watumishi 9,932 walibainika wakitumia vyeti bandia wakiwamo waliokuwa wakihudumia taasisi nyeti kama Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambayo watumishi wake 134 walikutwa na vyeti feki.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts