BOSI HALOTEL AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI | BONGOJAMII

BOSI HALOTEL AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viattel Tanzania (Halotel) Do Manh Hong, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.


Mshtakiwa Do Manh Hong amefikishwa mahakamani hapo na kuunganishwa na washtakiwa wengine saba waliofikishwa mahakamani hapo mapema Mwaka huu.


Wote kwa pamoja wanakabiliwa ma mashtaka kumi, kula njama. Kisimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutoa nyaraka za uongo, kusababisha hasara kwa serikali ya Tanzania, ya milioni 459, kutumia mitambo ya mawasilino ambayo haijathibitishwa na namba za simu.


Mbali na Hong, washtakiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka.


Kabla ya kusoma kwa mashtaka, wakili wa Serikali, Jehovanea Zacharias aliiomba mahakama kumuunganisha mshtakiwa Hong na kuwasomea washtakiwa wote makosa yao.


Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mshtakiwa Ahmed, Yaqoob, Mahamood, Ahmad, Anees, Kandasamy na Qammar Novemba 2016 Dar es Salaam walikula njama ya kutumia vifaa vya mtandao.


Imedaiwa kuwa, watuhumiwa walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila kibali cha TCRA.


Aidha imedaiwa kuwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na leseni na kuvisimika bila ya kuwa na kibali cha TCRA.


Imedaiwa, washtakiwa waliunganisha vifaa hivyo na huduma za mitandao kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya kuthibitishwa na TCRA.


Kwa upande wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited na Do Hong wanadaiwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria Kinondoni walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company Ltd kwa lengo la kusajili laini za simu 1000.


Kwa upande wa washtakiwa Ahmed na wenzake sita wanadaiwa kuwa Januari 5 ,2016 walitoa Cheti chakughushi cha usajili wa kodi chenye namba 100-864-210 kuonyesha imetolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati si kweli.


Mbali na mashtala hayo, watuhumiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuisababisha hasara TCRA na serikali ya Tanzania kiasi cha milioni 459.


Hata hivyo, washtakiwa wote hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mshtaka yanayowakabili yako nchini ya sheria ya uhujumu uchumi.


Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 29,2017.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts