HIVI NDIVYO NENO "ZUMBUKUKU" LILIVYOTAKA KUVUNJA BUNGE | BONGOJAMII

HIVI NDIVYO NENO "ZUMBUKUKU" LILIVYOTAKA KUVUNJA BUNGE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
NENO zumbukuku nusura livuruge Bunge juzi baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, kulitumia alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.


Profesa Kabudi alitumia neno hilo baada ya Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF), kumuomba Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, atoe ufafanuzi wa jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa salama wanapokuwa kazini.


Mbunge huyo alikitaja Kituo cha Televisheni cha Clouds kilichodaiwa kuvamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwalazimisha watangazaji waliokuwa studio, watangaze habari aliyokuwa nayo.


Pia alitaja tukio la waandishi wa habari kuvamiwa na kujeruhiwa walipokuwa kwenye mkutano ulioandaliwa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), Dar es Salaam.


“Nataka kupata maelezo ya Serikali juu ya aliyevamia Studio ya Clouds ili aliyevamia ajute kutokana na hatua alizochukuliwa na pia nataka mnieleze juu ya tukio la waandishi kuvamiwa wakiwa katika mkutano wa CUF,” alisema Mtolea.


Baada ya mbunge huyo kuwasilisha hoja hiyo na mjadala kuendelea, Profesa Kabudi aliomba kuweka sawa jambo hilo na kuwataka wabunge wasilijadili kwa sababu liko katika Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma ambako lilipelekwa na Meya wa Kinodoni, Boniface Jacob.


“Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekretarieti ya Maadili ya Umma inapofanya kazi yake, inakuwa na sifa ya mahakama.


“Sasa basi, tuache uzumbukuku na ndiyo maana shauri hilo litakaposikilizwa kwa mujibu wa kifungu cha 24, waziri wa habari ataitwa mbele ya baraza kwenda kutoa ushahidi na kuhojiwa.


“Kama masuala yaliyopekekwa yanahusu vyeti na maadili kama baadhi ya wabunge mlivyosema, sekretarieti ikikaa itayahoji yote hayo.


“Kwa hiyo sisi Bunge tukijadili jambo hilo, tunaharibu hiyo hoja, ndiyo maana tunasoma sheria miaka minne, tuache uzumbukuku, ndiyo, tuache uzumbukuku ‘this is a lecture room’,” alisema Profesa Kabudi.


Baada ya waziri huyo kukaa, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu (Chadema), alisema zumbukuku ni Profesa Kabudi mwenyewe na siyo wabunge wengine.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts