MAJIBU YA KAMANDA SIRO JUU YA KIJANA ALIYEUAWA AKIHISIWA KUWA NI JAMBAZI | BONGOJAMII

MAJIBU YA KAMANDA SIRO JUU YA KIJANA ALIYEUAWA AKIHISIWA KUWA NI JAMBAZI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetolea ufafanuzi malalamiko yaliyotolewa na ndugu za kijana aliyeuliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za ujambazi wiki moja iliyopita akidaiwa kujaribu kumpora askari silaha.


Kamishna Simon SirroKamanda wa jeshi hilo Kamishna Simon Sirro amewataka ndugu wa marehemu huyo wakatembelee eneo la tukio kusikia wananchi wanasema nini kuhusiana na kitendo cha kijana huyo ambaye aliuawa na polisi baada ya wenzake kukimbia kusiko julikana.


Amesema katika eneo la tukio palikuwa gari la kubebea fedha lililokuwa likisambaza fedha katika mashine za ATM za CRDB kiasi cha Tsh. 320, 000,00 ambapo mtuhumiwa huyo kwa kushirikiana na wenzake alidaiwa kutaka kufanya tukio la uvamizi katika gari hilo, kabla ya askari kumuwahi na kumuua.


Tangu kutokea kwa tukio hilo, ndugu wa marehemu huyo wamegoma kuchukua mwili wake kwa ajili ya maziko wakidai kuwa ndugu yao ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi wa UDSM hakuwa muhalifu, huku wakitaka jeshi hilo liombe radhi kwa kudai kuwa ndugu yao alikuwa mhalifu.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts