MBOWE AWANYOOSHEA KIDOLE LOWASA NA SUMAYE | BONGOJAMII

MBOWE AWANYOOSHEA KIDOLE LOWASA NA SUMAYE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameitaka serikali kuwachukulia hatua viongozi mbalimbali waliohusika katika kuliingizia serikali hasara ya mabilioni kutoka kwenye sekta ya madini.

Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro alitoa kauli hiyo katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA mjini Dodoma alipokuwa akizungumzia sakata la mchanga wa madini ambalo limepamba moto kwa sasa nchini.


“Tunafukuza watu kwa makosa yaliyofanywa miaka 15 iliyopita, lakini wale waliofanya makosa wapo uraiani, wapo huru” alinukuliwa Mbowe akizungumza.
Kwa kauli hii ya Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ni kuwa, baadhi ya waliokuwa viongozi wakuu wa shughuli za serikali wakati mikataba hii ikisainiwa na kazi hizi za usafirishaji wa mchanga ambao ni wananchama wa chama hicho, nao watachukuliwa hatua endapo serikali itaamua kuwashughulia wote waliohusika kwa namna yoyote.

Kama serikali ingekuwa inamchukulia kila mtu hatua tangu mikataba hii iliposainiwa, basi ni dhahiri Mawaziri Wakuu wasataafu Frederick Sumaye na Edward Lowassa ambao nao ni wanachama wa CHADEMA, kwa namna moja au nyingine wangehusika kwani wao pia walikuwa wasimamizi wa shughuli za serikali.

Mbali na jambo hilo lakini Mbowe alikikosoa pia Chama cha Mapinduzi kuwa kiliingia mikataba mibovu iliyopelekea nchi kupata hasara ya mabilioni. Mbowe alisema kuwa tatizo kubwa katika sekta ya madini ni sheria, ambazo wapinzani wamekuwa wakipiga kelele kila mara kuwa zirekebishwe.

Aidha, Mbowe aliwataka wanachama wa chama hicho kusimama kisawasawa na asiwepo mtu mwenye uwoga wa aina yoyote kwani wamedhamiria kushika dola mwaka 2020.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts