MVUA YA SIKU 6 , YAUA 10 NA KUBOMOA NYUMBA 44 | BONGOJAMII

MVUA YA SIKU 6 , YAUA 10 NA KUBOMOA NYUMBA 44

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Tanga. Tathmini ya madhara yaliyotokana na na mvua zilizonyesha kwa siku sita mfululizo wiki iliyopita mkoani hapa zimeonyesha kuwa hadi sasa watu 10 wamekufa huku nyumba 44 zikibomoka na nyingine 218 zikizingirwa na maji.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ametoa taarifa

ya tahmini hiyo leo, Jumanne wakati akizumgumza na waandishi wa habari jijini hapa.

Wakulyamba amesema katika yaliyotokena na mvua hizo, watu 10 walimepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, kuangukiwa nyumba na kutumbukia kwenye mashimo ambapo saba kati yao walikuwa wakazi wa Wilaya ya Korogwe, wawili Muheza na mwingine ni mkazi wa Jiji la Tanga huku 20 wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, nyumba 44 ziliezuliwa paa, 218 zilizingirwa na maji, 12 zikisombwa na mafuriko.

Amesema wilaya zilizoathirika zaidi ni Korogwe,Tanga na Lushoto huku Pangani,Mkinga

na Handeni zikipata athari ndogo.

Kamanda huyo alisema katika mafuriko hayo,barabara zilizopo katika za Wilaya mbalimbali mkoani Tanga,zimeathirika kwa kubomoka,kuvunjika makaravati pamaoja na madaraja.

"Kama mnavyoona mvua bado zinaendelea, nawatahadharisha wanaokaa kwenye nyumba zilizopo mabondeni wasisubiri maji yaingie ili waokolewe, kuna wakati mwingine uokoaji unaweza kutofanikiwa na kujikuta mnaangamia,"amesema Wakulyamba.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts