RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE WA BOSS TRA | BONGOJAMII

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE WA BOSS TRA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


Uteuzi wa Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru umeanza tarehe 22 Mei, 2017.


Kabla ya uteuzi huo Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.


Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts