SIMBA YATIBUA FURAHA YA UBINGWA WA YANGA, UTHIBITISHO HUU APA | BONGOJAMII

SIMBA YATIBUA FURAHA YA UBINGWA WA YANGA, UTHIBITISHO HUU APA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Ushahidi kuwa klabu ya Simba imewasilisha malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), umepatikana.

Kitendo cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na picha ikionyesha ushahidi huo, inaonekana kuwakwaza zaidi ya mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza sherehe za ubingwa.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwaita Simba “Wazee wa pointi za mezani”.

Lakini mashabiki wa Simba wamekuwa wakijibu mapigo na kusema, “Haki ni haki” na sheria itafuata mkondo wake.

Yanga na Simba zimemaliza ligi zikiwa na pointi 68 kila moja, lakini Yanga ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa GD.

Silaha ya Simba, inabaki kuwa suala la pointi za Kagera na kama kweli Fifa itaamuru irejeshewe, basi itafikisha pointi 71 na kutangazwa kuwa bingwa.

Simba ilishinda rufaa yake kupitia kamati ya Saa 72 ambayo ilibaini kuwa kweli beki Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano wakati Simba ilipolala kwa mabao 2-1 katika mechi ya ligi Kuu Bara.

Lakini Kagera Sugar ilikata rufaa katika kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji na kushinda ikarejeshewa pointi zake tatu.

Hata hivyo, wakati wa kutangaza kamati hiyo ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji haikutoa ufafanuzi wowote kuhusiana na Fakhi kama alikuwa na kadi mbili au tatu za njano.

Badala yake ikasema rufaa ya Simba ilichelewa pia haikulipiwa hivyo kuifanya iwe batili.

Lakini kuhusiana na pointi hizo tatu, inaonekana hata kama Simba isingekata rufaa na kama kweli Fakhi ana kadi tatu za njano, basi automaticaly, Kagera Sugar wangepokwa ushindi.

Hivyo, Simba imeamua kwenda Fifa kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa, basi moja kwa moja inatangazwa kuwa bingwa.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts