Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
WAHAMIAJI haramu wapatao 411 wamekamatwa katika kipindi cha miezi kumi kuanzia Julai 2016 mpaka Aprili 2017 kwenye maeneo tofauti ndani ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa wilaya hiyo Alhaj Hemed Mwanga ameitaja idadi hiyo kwenye Mkutano wa hadhara akizungumza na wananchi eneo la uwanja wa 77 nyuma ya Kituo cha Polisi cha Chalinze ambapo alisema, kuna watu wanaofadhili safari hizo hivyo ni vyema wakawataja ili wakamatwe na hatimae kudhibiti kabisa mtandao huo.
Alieleza kwamba katika kipindi hicho kifupi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya inapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi unaowezesha kuwakamata kwa wahamiaji hao wengiwao wakitokea nchi za Ethiopia na Somalia ambao aidha walikuwa wanapita njia au kujipenyeza kwa wananchi na kuweka makazi.
"Tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi kuhusiana na kuingia kwa wahamiaji hao, niwaombe ushirikiano huo uendelee, katika maeneo tunayoishi kuna watu wachache wanaofadhili safari hizo, tusiwafumbie macho tuwataje ili tudhibiti vitendo hivyo, athari yake ni kubwa endapo hatutatoa taarifa hizo," alisema Mkuu huyo.
Aidha alisema kuwa upande wa Bagamoyo wamefanikiwa kuudhibiti mtandao wa watu wanaojihusisha na kufadhili safari za wahamiaji hao, hivyo amewaomba upande wa Chalinze kutowafumbia macho kwani endapo wataendelea kuwapokea madhara yake ni makubwa.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka