WALPER NA HARMONIZE WAPIGANA CHINI | BONGOJAMII

WALPER NA HARMONIZE WAPIGANA CHINI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize Alhamisi alithibitisha kuachana na malkia wa filamu, Jacqueline Wolper.


Huenda wawili hao wamezinguana siku za karibuni, kwani Machi 16 mwaka huu Harmonize aliachia project yake ya wimbo ‘Niambie’ ambayo ndani yake Wolper alicheza vitendo na pia walishirikiana kwenye ishu ya promotion ya wimbo huo.


Akiongea katika kipindi cha Leo Tena, Harmonize amedai alikuwa na mipango mingi na Wolper lakini ameona bora aachane naye ili aupeshe shari.


“Sipo katika mahusiano, inshort kila mtu ana maisha yake ‘tumeachana'”alisema Harmonize .


Pia muimbaji huyo alikanusha taarifa za kwenye mitandao kuwa anatoka kimapenzi na msichana wa kizungu.


Hata hivyo hakuweka wazi sababu maalum ya kuachana na mpenzi wake huyo aliyedumu naye kwa muda mrefu pamoja na kumtambulisha kwao.


==>Msikilize hapo chini akiongea

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts