ALIKIBA ARUSHA JIWE GIZANI | BONGOJAMII

ALIKIBA ARUSHA JIWE GIZANI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Alikiba

Msanii Alikiba ambaye hivi sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kwenye Tamasha la 'OneAfrica Music festival' ambalo limefanyika siku ya Jumamosi ameamua kujibu mashambulizi kwa kushusha dongo pia kupitia mtandao wake wa Instgram.

Alikiba amefanya hivi siku moja baada ya hasimu wake katika muziki wa bongo kusikika katika moja ya wimbo ambao mashabiki wanahusisha baadhi ya mistari ya msanii huyo kwenda kwa Alikiba, ndipo hapo inasemekana Alikiba ameamua kujibu kwa kusema mfalme atabaki kuwa mfalme siku zote huku ikidaiwa akimfananisha hasimu wake na malkia wake.

Baada ya Alikiba kujibu mashambulizi hayo baadhi ya mashabiki wameonyesha kufurahishwa na kitendo hicho huku wengine wakimtaka Alikiba kuwa mpole na kumtaka yeye amjibu kwa kufanya kazi nzuri na kuonyesha ufalme wake katika muziki.

Kwa taarifa zilizopo zinasema kuwa Alikiba akirudi kutoka nchini Marekani atakuja kuachia kazi zake mpya, katika moja ya video ambayo inasambaa mitandaoni akiwa na msanii mwenzake Ommy Dimpoz walikuwa wakiimba wimbo wa CCM huki akibadili maneno na kusema wakirudi kutoka nchini Marekani wataisoma namba.


Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts