Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Promota na meneja maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Juma “Chief” Ndambile yupo katika mikakati ya kumleta nchini bondia maarufu wa ngumi za kulipwa duniani, Floyd Mayweather Jr, mara baada ya pambano lake Conor McGregor.
Floyd Mayweather Jr.
Awali, Mayweather alipanga kutembelea Ghana Juni mwaka huu, lakini safari hiyo iliharishwa ili kujiandaa na pambano lake dhidi ya McGregor lililopangwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu huko Las Vegas' T-Mobile Arena, Marekani.
Ziara ya Ghana kwa bondia huyo imeandaliwa na kampuni ya Upscale Entertainment ambapo mbali ya Ghana, bondia huyo alipanga kutembelea Nigeria.
Ndambile alisema jana kuwa amefanya mawasiliano na waandaaji wa ziara ya bondia huyo nchini Ghana na mazungumzo yanaendelea vizuri. Ndambile alisema baada ya kufanya mazungumzo ya awali, alilazimika kusafiri hadi Ghana ili kujadiliana jinsi ya kufanikisha ziara hiyo.
“Nilikwenda Ghana na kukutana na waratibu wa ziara hiyo, kuna mambo ambayo tulikubaliana nao kuhusiana na ziara hiyo, tunaendelea vizuri sana, tunasubiri pia menejimenti ya bondia huyo kutangaza tarehe rasmi ya kufika Ghana na masuala mengine yatafuata,” alisema Ndambile.
Ndambile alisema ameweka nia ya kufanikisha yale aliyoyapanga mara baada ya kuhudhuria mkutano mkuu wa Baraza la Ngumi za Kulipwa duniani (WBC) uliofanyika Desemba 11 hadi 17, mwaka jana nchini Marekani.
Tayari promota huyo amekabidhi taarifa ya mipango yake ya kuendeleza ngumi za kulipwa kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
“Nikiwa Marekani, niliweza kukutana na Rais wa WBC, Mauricio Sulaimai, pamoja na bondia Mayweather, mabondia Lenox Lewis, Amir Khan, Wladimir Klitschko, Evander Holyfield na mapromota maarufu kama Don King na Jay Mathews, wote hao wameonyesha nia ya kuja nchini kwa ajili ya kuona vivutio vya utalii na kuwekeza,” alisema Ndambile.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka