Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Papy Kabamba Tshishimbi.
YANGA jana ilianza kufaidi uwezo wa kiungo wao mpya, Papy Kabamba Tshishimbi baada ya kumshuhudia kwenye mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo dhidi ya Jamhuri ya Pemba, mechi iliyopigwa Uwanja wa Gombani, Pemba na kushinda kwa bao 1-0.
Kwa mara ya kwanza jana Jumapili, Tshishimbi alianza kuitumikia timu hiyo ya Yanga aliyojiunga nayo akitokea Mbabane Swallows ya Swailand, kwenye mchezo huo maalum wa kirafiki ambapo ni sehemu ya maandalizi yao kabla ya kuwavaa Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, keshokutwa Jumatano kwenye dimba la Taifa, Dar.
Licha ya kuingia kipindi cha pili cha mchezo huo na kutumia dakika 45 pekee, Tshishimbi aliweza kuonyesha uwezo mkubwa baada ya kupiga pasi 46, mashuti mawili, akifanyiwa madhambi mara mbili huku akitoka uwanjani bila ya kufanya faulo yoyote ile.
Kutokana na uwezo mkubwa aliounyesha Tshishimbi raia wa DR Congo ulisababisha mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza uwanjani hapo kumshangilia kwa kila kitu ambacho alikuwa anafanya.
Lakini pia Tshishimbi ambaye ana siku mbili tu tangu ajiunge na wenzake kwenye kambi hiyo ya Pemba, alionyesha kuelewana kwa kiasi kikubwa na Mzimbabwe, Thaban Kamusoko aliyecheza naye kwenye kiungo cha timu hiyo na kuchangia kuwavuruga wapinzani wao.
Nahodha na beki kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alimzungumzia kiungo huyo mpya kwa kusema: “Ni mchezaji mzuri na atasaidia kuongeza hamasa kwetu, kwa hiyo niwaambie wapinzani wetu wajiandae kwa kichapo.”
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka