FOD Q APINGANA NA KAULI YA WAZIRI MWAKYEMBE | BONGOJAMII

FOD Q APINGANA NA KAULI YA WAZIRI MWAKYEMBE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii Fareed Kubanda ambaye wengi humuita 'Fid Q', amejibu kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe aliyosema wasanii wasiimbe siasa, na kusema kuwa siyo rahisi kwa wasanii kuacha kitu kitu hicho.

Fid Q amesema Waziri hakuwa sahihi kusema hivyo, kwani siasa ipo kwenye maisha yetu ya kila siku, ambayo wasanii ndiyo kitu ambacho hutazama ili kuweza kufanya kazi zao.

"Nafikiri suala la Waziri wa Habari kusema wasanii wasiimbe siasa halikuwa sahihi, nafikiri labda alitaka kusema wasanii wasiwaimbe wanasiasa, kwa sababu siasa ni sehemu ya maisha yetu, na tunaguswa nayo kwa namna moja au nyingine, tunataka au hatutaki, na sanaa ni kitu ambacho hakina mipaka ili mradi hujavuka mstari, na kazi ya msanii ni kuelimisha jamii si tu kuburudisha", alisema Fid Q.

Fid Q aliendelea kusema kuwa hata mafanikio ambayo Mh. Waziri aliyazungumzia, anatakiwa atambue kuwa msanii kufanikiwa sio kuwa na mali tu, hata kubadilisha jamii kupitia sanaa yake ni mafanikio makubwa.

"Bob Marley aliimba siasa mpaka leo tunatambua legacy yake inaendelea kuishi, Fela Kuti pia, alafu mafanikio ya msanii siyo lazima masuala ya pesa, magari sijui majumba, mafanikio kwa msanii ni namna sanaa yake inaweza kubadilisha jamii, na kuamini kwamba pesa, magari na nyumba za kifahari ndiyo vitu vya mafanikio, si nadharia nzuri na yenye busara kwenye jamii", alisema Fid Q.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts