Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mwenyekiti wa Taifa wa ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, ametoa rai hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kauli za uchochezi zenye kuweza kulewa mpasuko ndani ya chama chake hazikubaliki.
Kauli hiyo Mhe. Rashidi imedhaniwa kuwa huenda ikawa inamlenga Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ambaye mara kadhaa amenukuliwa akiahidi kushika wadhifa wa Rais wa Zanzibar.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa ADC Bw. Doyo Hassan Doyo, amevitaka vyama vingine vya upinzani kujenga tabia ya maridhiano pamoja na kusameheana, kama njia ya kumaliza migogoro inayoendelea ndani ya vyama hivyo, kama ambavyo ADC imefanya hivi karibuni kwa kuwasamehe wanachama wake ambao walifukuzwa uanachama miaka michache iliyopita.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka