MAKAMANDA WA ZIMAMOTO WAPANGULIWA | BONGOJAMII

MAKAMANDA WA ZIMAMOTO WAPANGULIWA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa na wakuu wa vitengo wa jeshi hilo. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari na Elimu kwa Umma cha Jeshi hilo kwa vyombo vya habari jana, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi (ACF) Bakari Mrisho, amekuwa Mkuu wa Chuo na Mafunzo nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu (SF) Kennedy Komba, ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Iringa huku nafasi yake ikichukiliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF), James John toka Makao Makuu.

Kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi (ACF) Gilbert Mvungi, amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Baraza Mvano, ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma.

Kamanda wa Viwanja vya Ndege Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Kwiyamba amehamishiwa Makao Makuu huku nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Christom Manyologa. 

Taarifa iliongeza kuwa Kamishna Msaidizi (ACF) Fikiri Salla amekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mbeya na anajaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya kuteuliwa na Rais ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Dk. John Magufuli, kuwa Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto.

Katika mabadiliko hayo, Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Mrakibu Msaidizi (ASF) Goodluck Zelote amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Tanga. Nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Happy Shirima kutoka Makao Makuu.

Mrakibu Msaidizi (ASF) Fatma Ngenya amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Manyara kuchukua nafasi ya Mkaguzi Msaidizi (A/INSP) Heriel Kimaro, ambaye amehamishiwa Makao Makuu.

Taarifa ilifafanua kuwa uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts