KESI YA LEMA YAMKERA JAJI , MAWAKLILI WA JAMHURI WASHINDWA KUFIKA | BONGOJAMII

KESI YA LEMA YAMKERA JAJI , MAWAKLILI WA JAMHURI WASHINDWA KUFIKA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Dk. Modester Opiyo, amekerwa na kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, kutokana na tabia ya mawakili wa Jamhuri kutofika mahakamani. 


Godbless Lema. 

Kutokana na mawakili hao kutofika mahakamani na kukwamisha usikilizwaji wake, Jaji Opiyo amewataka kuacha tabia hiyo.

Dk. Opiyo aliyasema hayo jana mahakamani hapo, akishangaa kwa nini anaanza kesi bila kuwapo mawakili wa Jamhuri.

Alisema rufani ya mbunge huyo ambayo imefunguliwa mahakamani hapo kupinga uamuzi mdogo uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kuhamasisha watu kukusanyika na kufanya maandamano ya Ukuta kinyume cha sheria, inashangaza kuona upande wa Jamhuri kutohudhuria.

Alimhoji wakili wa Lema, Sheck Mfinanga, sababu za mawakili wa Jamhuri kutokuonekana mahakamani na kuahirisha kesi kwa muda kisha kumtuma wakili huyo kuwaangalia mawakili hao, Khalili Yuda na Innocent Njau ili waingine mahakamani kuiwakilisha Jamhuri katika rufani hiyo. 

“Kesi hii ina muda mrefu mahakamani hapa, mara ya mwisho nyie mawakili mlikuja mwezi Machi mwaka huu kisha tukaahirisha kesi, mara kwa mara tunaahirisha na leo tena mnataka niahirishe, hapana,” alisema Jaji Opiyo.

Baada ya muda mawakili hao ambao awali walikuwa na kesi nyingine mahakamani, walifika na kumuomba Jaji Opiyo kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27, mwaka huu.

Jaji Opiyo alisema kesi hiyo itasikilizwa kwa njia ya maandishi ambapo Agosti 30 upande wa Lema utawasilisha hoja zao (maombi yao) na Septemba 13 upande wa Jamhuri utajibu hoja hizo kisha Septemba 20 kutakuwa na usikilizwaji wa hoja hizo na uamuzi utatolewa Septemba 27, mwaka huu.

Awali, wakili wa Lema, Mfinanga alitaka kesi hiyo isikilizwe na Mahakama ya Katiba (Mahakama Kuu) mbele ya jopo la majaji watatu kutokana na kuwa na masuala ya kikatiba kwenye hati ya mashtaka.

Rufani hiyo mwanzoni ilipangwa kuanza kusikilizwa Julai 12, mwaka huu na Jaji Dk. Opiyo, lakini baada ya Wakili John Mallya anayemtetea Lema, kuieleza mahakama hiyo hawajajipanga kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo kwa maelezo kuwa walijua kesi ilikuwa imepangwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Mallya aliiomba mahakama hiyo kuahirisha rufani hiyo na kuipangia tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa mawakili hao kuwasilisha hoja zao za rufani.

Jaji Dk. Opiyo alikubaliana na ombi hilo la makili huyo na kuahirisha rufani hiyo hadi jana.

Februari 8, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilitoa uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na mawakili wa Lema,katika kesi ya jinai namba 352/2016 mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Bernard Nganga, ambaye alitupilia mbali pingamizi hiyo na kusema mahakama hiyo ina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts