MCT WAMTIA HATIANA RC MAKONDA | BONGOJAMII

MCT WAMTIA HATIANA RC MAKONDA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limezidi kumkaanga Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Mkaonda baada ya kubaini kwamba alihusika moja kwa moja kuvamia Clouds Media Group, anaandika Faki Sosi.


Mwezi Machi mwaka huu, Tume maalum iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ilitoa ripoti kama ya MCT.

Katika ripoti yake, MCT imebaini Makonda alihusika kufanya uvamizi huo na wamejiridhisha pasipo kuacha shaka na kwamba hawajamuonea.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema kuwa ripoti hiyo hajamuonea Makonda.

“Hatujafanya utafiti huu kwa sababu tunamahaba maalum na Clouds au tunamahaba na mkuu wa mkoa na kwamba huu sio utafiti wa kwanza tulianza kwa marehemu Daudi Mwangosi alipouwa,” amesema

”Sisi kwetu haijarishi watu wameelewana au hawajaelewana sisi kwetu tunaangalia uvamizi huu jinsi ilivyoathiri vyombo vya habari”, amesema Mukajanga

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts