MEYA WA KINONDONI AIKINGIA KIFUA SERIKALI | BONGOJAMII

MEYA WA KINONDONI AIKINGIA KIFUA SERIKALI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ameeleza kuwa licha ya serikali kuu kuchukua baadhi ya vyanzo vya mapato vya Halmashauri hiyo ikiwemo Kodi ya Bango, Huduma, na Majengo, halmahauri hiyo inataraji kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ili iweze kusimamia baadhi ya miradi ya manispaa hiyo.


Meya Sitta ameongeza kuwa pamoja na vyanzo hivyo vya mapato kuchukuliwa na serikali lakini imekuwa ikiwasaidia kulipa baadhi ya fidia ikiwemo fidia ya mradi wa DMDP ambapo serikali imeilipia Manispaa kiasi cha shilingi bilioni moja. 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Aron Kagurumjuli ameeleza kuwa vyanzo vya mapato vilivyochukuliwa na serikali kuu, serikali imeamua kukusanya mapato kwa niaba ya Halmashauri. 


Huku Mbunge wa Kawe Halima Mdee ameitaka serikali kuhakikisha inapofanya marejesho ya mapato ya vyanzo vya Halmashauri ilizo zichukua kwa kiwango kinachoridhisha ili Halmashauri iweze kuendesha miradi yake ipasavyo.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts