MSUVA AZIDI KUNG'AA AFUNGA MAGOLI SITA KATIKA MECHI NANE | BONGOJAMII

MSUVA AZIDI KUNG'AA AFUNGA MAGOLI SITA KATIKA MECHI NANE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefikisha mabao sita ya kufunga tangu amejiunga na Difaa Hassani El-Jadida (DHJ) ya Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola.

Hiyo inafuatia Msuva jana kufunga bao moja katika mechi yake nane DHJ ikifungwa 2-1 na timu ya Daraja la Kwanza, Union Sportive Musulmane Oujda (USMO) Uwanja wa El Abdi mjini Jadida.

“Jana nimefunga tena, hilo ni bao langu la sita sasa katika mechi nane zote za kirafiki. Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na hapa kila siku ninachojua ni bidii tu ili nitimize malengo yangu,”amesema Msuva akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo.

Msuva alisaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na DHJ Julai 28, mwaka huu baada ya kucheza Yanga ya nyumbani, Tanzania tangu mwaka 2012 akitokea Moro United iliyokuwa tayari imehamishia maskani yake Dar es Salaam kutoka Morogoro.

Awali ya hapo, Msuva alipitia akademi ya Azam akitokea kituo cha kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi, Wakati Ujao baada ya kuibuliwa na iliyokuwa taasisi ya Pangollin ya kocha Charles Boniface Mkwasa, ambaye sasa ni Katibu wa Yanga, klabu aliyoichezea na kuifundisha awali..

Na baada ya kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mfungaji bora mara mbili – Msuva amehamia Morocco kusaka changamoto mpya na mafanikio zaidi kisoka.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts