MVUA KUBWA ZALETA MAAFA NA VIFO SIERRA LEONE | BONGOJAMII

MVUA KUBWA ZALETA MAAFA NA VIFO SIERRA LEONE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, imeongezeka na kufikia zaidi ya watu mia tatu.

Jitihada za kuokoa zilisitishwa kwa muda baada ya giza kuingia, Rais Ernest Bai Koroma amesema kupitia televisheni kwamba vituo vya dharura vimewekwa ili kukabiliana na kile alichokiita janga la taifa.

Shirika la Msabala mwekundu limesema inakadiriwa zaidi ya watu laki tatu wamepoteza makazi yao.
Eneo lililoathirika zaidi wilaya ya Regent iliyopo pembezoni mwa mji wa Freetown baada ya mlima uliojaa maji kuporomoka.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts