NAY WA MITEGO AWAPA ZA USO WOTE , DIAMOND , ALIKIBA NA DIMPOZ | BONGOJAMII

NAY WA MITEGO AWAPA ZA USO WOTE , DIAMOND , ALIKIBA NA DIMPOZ

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Ommy Dimpozi kupost picha akiwa na mama mzazi wa Diamond imechukua sura mpya baada ya watu wengi kuipokea kwa hisia tofauti hasa wakilinganisha na maneno yaliyoambatana na picha hiyo na hali ilivyo sasa baina ya mastaa hao.

Mmoja wa walioipokea kwa hisia tofauti ni staa mwingine wa Bongofleva Nay Wa Mitego ambaye baada ya kuiona na kuisoma post ya Ommy Dimpoz aliandika kwenye Instagram yake akitoa angalizo kwa watu kutohusisha wazazi kwenye migogoro yao binafsi.

Nay Wa Mitego kaandika”Gombaneni, Loganeni Mpaka Muuwane… Napenda Kusikia Challenge Kwenye Game, Ila Tusiwaingize Wazazi Wetu🙏🏿 Please. Tutukananeni Matusi Yote Wenyewe Kwa Wenyewe Ikibidi Piganeni Kabisaaaa Atakae Kufa Tutazika na Itakua Historia Kama Big na Pac. Ila Kuwaingiza Wazazi ni…

“Sipo Upande Wowote, Si #Kiba #MondWala #Ommy. Endeleeni na Vita yenu Kama Wanawake Mmechukuliana Mabwana. Ila Swala la Wazazi Mnavuka Mipaka” – Nay wa Mitego

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts