OKWI ATAMBA KUPELEKA MSIBA JANGWANI LEO | BONGOJAMII

OKWI ATAMBA KUPELEKA MSIBA JANGWANI LEO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.
STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi, juzi alifunguka kuwa anataka kuwanyamazisha wapinzani wao, Yanga kwa kuwapelekea kilio wakati watakapovaana leo Jumatano kwenye pambano la Ngao ya Jamii.

Okwi amejiunga na Simba kwa mara ya tatu tangu alipoanza kuichezea timu hiyo akitokea katika Klabu ya SC Villa ya Uganda kwa mkataba wa miaka miwili, amekuwa na wakati mgumu tangu alipojiunga na timu hiyo kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa wakidhihaki kiwango chake.

Akizungumza na Championi Jumatano, Okwi alisema kwamba kila jambo linalotokea uwanjani hupangwa na Mungu, hivyo hakuna anayeweza kutambua mbinu za mwenzake au kiwango chake zaidi ya Mungu, kwa maana hiyo anayeona ana upungufu, basi dakika 90 zitajibu.

“Watu wanachotakiwa kujua ni kwamba mimi nipo hapa kwa ajili ya kupiga kazi, majibu ya kazi yangu yatabaki uwanjani na si nje ya uwanja kwani mpira siyo sarakasi bali ni mchezo unaoamuliwa na dakika 90.
“Labda niwaambie tu kuwa nitapeleka kilio kwa wapinzani wetu Yanga na kufanikisha suala la kuwapa raha mashabiki wetu, lakini nawaambia waje watupe sapoti,” alisema Okwi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts