Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Kocha wa timu ya Simba, Joseph Omog.
WAKATI homa ya mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga ya Agosti 23, mwaka huu ikizidi kukolea huku timu hizo zikiwa kisiwani Zanzibar kujifua, rekodi zinaonekana kuwa nzuri upande wa Yanga.
Yanga ikiwa Pemba wakati Simba ipo Unguja, kuna taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa kuna baadhi ya memba wameanza kuhofia rekodi ya timu hizo zinapokutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
“Kocha (Joseph Omog) alishtuka baada ya kuiona rekodi ya Yanga ya Ngao ya Jamii tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 2001.
“Unajua Yanga ndiyo timu pekee iliyofanikiwa kuichukua Ngao mara nyingi, kocha anaumiza kichwa kuivuruga rekodi yao hiyo,” kilisema chanzo cha habari.
Rekodi zinaonyesha Yanga imecheza mechi nane na kubeba Ngao mara tano wakati Simba imecheza mechi nne na kuchukua Ngao mara mbili. Azam FC imecheza mara tano na kutwaa mara moja sawa na Mtibwa Sugar ambayo imecheza mara moja na kutwaa mara moja.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka