SERIKALI YA ZIMBABWE KUINGILIA KATI KESI YA MKE WA ZIMBABWE | BONGOJAMII

SERIKALI YA ZIMBABWE KUINGILIA KATI KESI YA MKE WA ZIMBABWE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Serikali ya Zimbabwe imemuombea Mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe kinga ya kidplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na maofisa wa polisi wa taifa hilo leo asubuhi zimedai kuwa hayo yamefanyika kwa mujibu wa sheria, huku wakisisitiza kwamba mwana mama huyo bado yupo Afrika ya Kusini huku wakipinga ripoti za awali zilizosambaa kwamba Grace Mugabe alikuwa amerudi nchini Zimbabwe.


Akizungumza mbele ya kamati ya bunge mapema, Kaimu Mkuu wa Polisi Lesetja Mothiba (Afrika Kusini) alisema kuwa Grace Mugabe anatakiwa aende mahakamani kulingana na sheria.


Taarifa za awali zinasema kuwa Bi Mugabe anadaiwa kutenda kosa la kumshambulia mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 katika hoteli jijini Johannesburg Afrika ya Kusini baada ya kumkuta na wanae alioko masomoni Afrika Kusini.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts