SHULE 125 ZABAINIKA KUWA FEKI | BONGOJAMII

SHULE 125 ZABAINIKA KUWA FEKI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam imeanza zoezi la kuzifungia Shule binafsi za msingi na za awali zipatazo 125 kwa kuendeshwa kinyume cha sheria ikiwemo kukosa usajili na kutokuwa na eneo la kutosha kuendeshea shule hizo.

Afisa Elimu wa shule za msingi katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi. Elizabeth Thomas amesema kuwa, mpaka sasa wamezifungia shule zaidi ya 25 huku wakibaini mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na baadhi ya shule kubandika namba ya usajili feki wakati haikusajiliwa, kukosa vyoo na vingine zikijiendesha kinyume cha utaratibu.

Akitaja Baadhi ya shule zilizokwisha kufungwa kuwa ni pamoja na Mbingaa Nursery & Primary school English Medium, Montessori Nursery School & Proficience College Ilala, Morning Star,Gift Academy, New Generation na nyingine nyingi

Aidha Afisa huyo amewataka wazazi kujenga tabia ya kufuatilia usajili wa shule kabla ya kuwandisha watoto ao ilikuepuka usumbufu unaojitokeza baada ya shule hizo kufungiwa

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts