Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Jeshi la Polisi nchini linapenda kuutaarifu umma kwamba linatarajia kuwaaga Makamishna wa Jeshi la Polisi watatu (3), ambao wamefikia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria kwa kutimiza miaka sitini (60) katika utendaji wao wa kazi.
Makamishna hao waliostaafu Julai, 2017 ni pamoja na aliyekuwa Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, aliyekuwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame na aliyekuwa Kamishina wa Tume ya kudhibiti dawa za kulevya Kenneth Kasseke.
Hafla hiyo itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 18/08/2017 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA), kilichopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es eSalaam kuanzia Saa Moja (7.00) Asubuhi. Wananchi wote pamoja na waandishi wa habari mnakaribishwa.
Katika utumishi wao uliotukuka ndani na nje ya Jeshi la Polisi walishika nyadhifa mbalimbali na kuliletea sifa Jeshi la Polisi ndani na nje ya nchi. Kama tunavyofahamu kuwa uhalifu hauna mipaka, wameshiriki kikamilifu katika operesheni mbalimbali za kitaifa, kikanda na kimataifa.
Kutokana na mchango wao kwa taifa wametakiwa kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi wakati wowote watakapo hitajika kutoa ushirikiano wa namna yoyote ili kusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini kwasababu suala la usalama ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.
Aidha, tunaamini watakuwa mabalozi wa Jeshi la Polisi Tanzania hususani katika kipindi hiki cha ushirikishwaji wa wananchi katika suala la ulinzi na usalama nchini mahali popote watakapokuwa wakiendelea na shughuli zao za kila siku baada ya kustaafu.
Imetolewa na:-
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
17/08/2017
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka