WAJUMBE WAPYA KAMATI YA TFF KUWEKWA HADHARANI JUMAMOSI | BONGOJAMII

WAJUMBE WAPYA KAMATI YA TFF KUWEKWA HADHARANI JUMAMOSI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
RAIS MPYA WA TFF, WALLACE KARIA.
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inatarajia kukutana keshokutwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali muhimu ikiwamo kuteua wajumbe watakaounda kamati zitakazosimamia shughuli za shirikisho hilo.

Kikao hicho cha Jumamosi kitakuwa ni cha pili cha kamati hiyo iliyoingia madarakani Agosti 12 mwaka huu, baada ya kile cha utambulisho kilichofanyika Dodoma Jumapili iliyopita.

Rais mpya wa TFF, Wallace Karia, ambaye aliwashinda wapinzani wake kwa kupata idadi kubwa ya kura ndiye anatarajiwa kuongoza kikao hicho.

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya shirikisho hilo zinaeleza kuwa pia Karia huenda akawasilisha majina ya wajumbe wawili wa kuteuliwa watakaoingia kwenye kamati hiyo.

"Katiba inamruhusu Rais kuteua wajumbe wa kamati ya utendaji watatu, ila atatakiwa kuleta kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kupata baraka na baadaye watatangazwa," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji.

Kikao hicho pia kinatarajiwa kujadili hatima ya wafanyakazi walioajiriwa katika shirikisho hilo ambalo mikataba yao imemalizika na baadhi yao wakidaiwa kutokuwa na sifa zinazostahili kwenye vyeo wanavyovifanyia kazi.

Mbali na Karia, viongozi wengine waliochaguliwa katika uchaguzi huo uliopita ni pamoja na Makamu Rais, Michael Wambura, huku wajumbe wa Kamati ya Utendaji wakiwa ni pamoja na Lameck Nyambaya, Francis Ndulande, Issa Bukuku, Mohamed Aden, Sarah Chao, Vedastus Lufano, Mbasha Matutu, Saluom Chama, Keneth Pesambili, Elias Mwanjala, James Mhagama, Dustan Mkundi na Khalid Mohamed.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts