Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Juzi kulipigwa pambano kati ya timu ya taifa ya Hispania dhidi ya timu ya taifa ya Italia, mchezo ulipigwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu na ikishuhudiwa timu ya taifa ya Hispania ikiibuka na ushindi wa bao 3 kwa 0.
Gumzo kubwa katika mchezo huo ilikuwa kiwango kilichooneshwa na kiungo wa timu ya Real Madrid ambaye anakipiga Hispania Isco ambaye ndiye alikuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Isco alionekana kuinyanyasa Italia atakavyo huku kiungo wa PSG Marco Veratti akiwa mhanga mkubwa wa mabalaa ya Isco ambapo mara nyingi Veratti aluonekana kushindwa kumzuia Isco afanye anachotaka.
Baada ya mchezo kuisha Veratti aliongea kitu kuhusu mchezo huo na kukiri kwamba alishindwa kumzuia Isco na anaamini kwa kiwango cha Mhispania huyo siku ya jana hata Lioneil Messi asingeweza kumgusa.
“Nilihangaika na kupata tabu sana kumzuia Isco, kiwango chake kilikuwa kiko juu sana na hata Lioneil Messi hafikii kiwango alichokionesha Isco dhidi yetu” alisema Veratti ambaye kipindi cha pili alipigwa tobo na Isco lilizua gumzo mitandaoni.
Hispania bado wanaendelea na kampeni yao ya kufudhu kombe la dunia ambapo Jumanne watacheza dhidi ya Albania kabla ya kwenda kucheza dhidi ya Israel mwezi ujao.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka