YANGA KUSHUSHA KIFAA KINGINE | BONGOJAMII

YANGA KUSHUSHA KIFAA KINGINE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
KOCHA wa Yanga, George Lwandamina, ametua tangu usiku wa kuamkia jana akitokea kwenye msiba wa baba yake. Habari mpya ni kwamba ameiambia klabu hiyo iongeze mtaalamu mwingine kwenye benchi la ufundi.


Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina
Alichogundua Lwandamina katika kikosi chake ni kwamba washambuliaji wake watatu; Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Geofrey Mwashiuya, walikuwa na majeruhi kwa muda mrefu wakiuguza tatizo la aina moja, maumivu ya magoti.

Habari za uhakika ambazo Lwandamina mwenyewe kathibitisha ni kwamba kocha huyo ameomba kutafutiwa mtaalamu wa matibabu ya viungo atakayesaidiana na daktari wa timu hiyo Dk. Edward Bavu.

Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema tayari maombi hayo ambayo hata wao wameyakubali, yameshaanza kufanyiwa kazi kwa kumtafuta mtaalamu huyo kwa kuangalia ndani na nje ya nchi atakayefanya kazi hiyo.

Lwandamina alisema: “Nikweli nimewaomba wanitafutie huyo mtu, sawa sasa tuna daktari wa timu lakini tunatakiwa sasa kufikiria mbali zaidi kumaliza hali kama hii ya kuwa na wachezaji wengi muhimu majeruhi kama hivi na hili linaweza kuwa tatizo zaidi unapokuwa katika mashindano makubwa ya Afrika ambayo hayana muda wa kupoteza kila mchezo ni muhimu.”

SMG naye anukia
Wakati Lwandamina akiwasilisha ombi hilo, taarifa zaidi zinasema pia mabosi hao walikuwa na mpango wa kumuongeza winga wa zamani wa timu hiyo, Said Maulid ‘SMG’ ambaye ni mtaalamu wa kukusanya takwimu mbalimbali za wachezaji.

SMG ambaye sasa yuko nchini baada ya kumaliza kazi yake hiyo huko Angola, ameliambia Mwanaspoti kuwa ingawa bado Yanga hawajamfuata, lakini yuko tayari kufanya kazi hiyo akiwa na Yanga ili aweze kusaidia kuboresha viwango vya wachezaji wa timu yake hiyo ya zamani.

“Kwa sasa nipo nchini, Yanga hawajanifuata rasmi katika hilo, lakini niseme tu hii ni timu ya hapa nyumbani siwezi kuwakatalia kama wakiona kuna kitu naweza kuwasaidia hawa wachezaji wetu,” alisema.

“Nimemalizana na klabu yangu ya kule Angola nimeona nipumzike kidogo, lakini kama Yanga wataona nitawafaa nipo tayari kuwafanyia kazi, nipo vizuri katika hili.”

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts