OKWI ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI AGOST | BONGOJAMII

OKWI ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI AGOST

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemchagua mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inaendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali.

Taarifa hizo zimetolewa na Shirikisho hilo mchana wa leo na kusema wamefikia hatua hiyo baada ya Okwi kuwashinda wenzake wawili ambao ni Mohamed Issa (Mtibwa Sugar) pamoja na Boniphace Maganga (Mbao FC) katika uchambuzi uliofanywa Jijini Dar es Salaam jana (Jumatano) na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha wa viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa.

Kwa mujibu wa TFF wachezaji wote timu zao zilifanikiwa kushinda katika michuano ya Ligi Kuu kwa michezo iliyopita round ya pili.

Kwa upande mwingine, timu ya Simba itashuka dimbani Septemba 17 (jumapili) kuivaa Mwadui FC katika kiwanja cha Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts