Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Umoja
wa Mataifa unaichunguza Tanzania kwa tuhuma za kikuikwa vikwazo vya
kisilaha ilivyoiwekea Korea Kaskazini ambapo inadaiwa kuwa licha ya
vikwazo vilivyowekwa, Tanzania imeendeleza biashara ya silaha na nchi
hiyo..
Ripoti
ya Septemba 9 ilitolewa siku mbili kabla ya Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa kwa pamoja kuweka vikwazo vipya vinavyo ishinikiza Korea
Kaskazini kufanya mazungumzo juu ya silaha zake za nyuklia.
Jopo
la watu wanane limesema linafanya tathmini juu ya taarifa kutoka kwa
vyanzo vya habari vya nchi wanachama wa UN ambavyo havijatajwa majina
vikisema kuwa Tanzania iliingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini
yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 12.5.
Kampuni
ya Haegeumgang Trading Corporation ya Korea Kaskazini inasemekana kuwa
inafanya ukarabati na kurekebisha mifumo ya makombora ya kivita nchini
Tanzania na ulinzi wa anga ( Rada) kuifanya iwe ya kisasa.
“Serikali ya Tanzania mpaka sasa bado haijatoa maelezo kujibu mambo ambayo yamedadisiwa na jopo hilo,” wachunguzi wa UN wamesema.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dr. Suzan Kolimba amesema kuwa hawajapokea taarifa yoyote kutoka UN na hivyo kwa sasa hawawezi kuzungumza kuhusu madai hayo yaliyotolewa.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dr. Suzan Kolimba amesema kuwa hawajapokea taarifa yoyote kutoka UN na hivyo kwa sasa hawawezi kuzungumza kuhusu madai hayo yaliyotolewa.
Mbali
na Tanzania, mataifa mengine yanayochunguzwa na UN ni kwa kuendeleza
biashara na Korea Kaskazini ni Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC), Eritrea, Msumbiji, Namibia, Syria na Uganda.
Korea
Kaskazini imekuwa ikiwekewa vikwazo mbalimbali siku za karibuni
kutokana na kuendelea na majaribio ya silaha za nyuklia kinyume na
makubaliano ya UN.
Kiongozi
wa nchi huyo, amewahi kunukuliwa akisema kuwa nchi hiyo kwa sasa ina
makombora makubwa yanayoweza kulenga sehemu yoyote ya dunia
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka