Miaka Mitano Baada ya Kufariki,Huu Hapa Ukweli Juu ya Kifo cha Patrick Mafisango kwa Saa 24 Kabla na Baada ya Ajali.. | BONGOJAMII

Miaka Mitano Baada ya Kufariki,Huu Hapa Ukweli Juu ya Kifo cha Patrick Mafisango kwa Saa 24 Kabla na Baada ya Ajali..

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD



USIKU wa Jumanne ya Aprili 15, 2012 vijana wawili wachezaji wa soka wanabishana kuhusu kuondoka mahali walipokuwa ili wakapumzishe miili yao baada ya pirika za kutwa nzima. Hao ni viungo wa soka, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ na Patrick Tabu Mutesa aliyekuwa maarufu kama Patrick Mutesa Mafisango ambaye kwa sasa ni marehemu.



Kwa mujibu wa Redondo, Mafi sango alitaka waendelee kukaa katika klabu moja ya usiku kwa muda kidogo lakini kwa kuwa ilishakuwa usiku sana yapata saa 7:00, yeye alimsihi waondoke na kweli wakaondoka. Haikuwa rahisi kwa Mafisango kuondoka mahali hapo lakini ushawishi mkubwa wa Redondo uliwezesha wawili hao kuondoka na kurudi nyumbani kupumzika.Wachezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mafisango.



KIONGOZI SIMBA ATOA FEDHA



Asubuhi ya Jumatano Apri- l i 16, 2012 akiwa ny- umbani kwake Chang’ombe jijini Dar es Salaam, Mafi sango aliletewa fedha na kiongozi mmoja wa Simba kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Baada ya kupokea fedha hizo, Mafisango akiwa na Redondo alianza kulazimisha waanze kupata ‘moja moto moja baridi’ lakini mwenzake alikataa hadi watakapopata chakula cha mchana.



“Alionekana kutaka kinywaji sana lakini nilimsihi kwamba si vizuri kutumia kinywaji muda huo badala yake asubiri hadi tutakapopata chakula cha mchana kwanza,” anasema Chombo. Baadaye Mafi sango aliletewa gari Toyota Chaser GX 100 kwa ajili ya kulitumia siku hiyo, lakini mpwa wake Orly Ilemba na Ally Hassan ‘Bozy’ walitoka na gari hilo kwenda Magomeni. Baada ya kuwasubiri kwa muda mrefu, Mafi sango na Redondo waliamua kuwafuata Magomeni akina Orly baada ya kuona wanachelewa kurejea Chang’ombe na gari hilo.Lari lakebaada ya ajali.



MAFISANGO APIGA USINGIZI WA AJABU



Walipofi ka Magomeni, Mafi sango na Redondo waliungana na akina Orly kisha wakalekea Kinondoni ambako walipata chakula lakini jambo la kushangaza baada ya kula, Mafi sango alilala usingizi mzito. “Wakati analala nikawaambia watu tuliokuwa nao kwamba wamuache apumzike na alilala usingizi mzito sana hadi alipozinduka baada ya kama saa mbili hivi,” anasema.



Kabla ya kula Mafi sango aliwarushia maneno akina Orly ambao hawakuonyesha hamu ya kula chakula hasa baada ya kuwasema kwa kuchelewa kuwafuata Chang’ombe.AGAWA FEDHA NA KUAGA



Karibu muda mwingi wa mchana, Mafi sango alikuwa akitoa fedha au vinywaji kwa watu huku akisema kwa utani, kunyweni hamjui labda ndiyo tunaagana au maisha haya mafupi sana. Hata fedha alikuwa akitoa kwa baadhi ya watu aliokuwa akifahamiana nao na karibu wote alikuwa akiwapa na kuwaambia maneno hayo.


“Sisi tuliona kama kitu cha kawaida lakini kumbe yeye sijui kuna kitu alihisi au la, lakini alikuwa akitoa fedha na kutamka maneno ya kuaga,” anasema Bozy.SAFARI YA MAISHA CLUB



Mafisango alikuwa na asili ya DR Congo licha ya kuwa na uraia wa Rwanda, alihamia Rwanda akiwa mkubwa na ni katika harakati za maisha ya soka tu. Huko ndiko alikopata jina la Mafi sango ambalo ni la ukoo wa mwanamke aliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Crespo, hivyo Mafi sango alitumia jina la mkwewe.



“Safari ya kwenda Maisha Club ilianzia katika Pub moja iliyopo Kinondoni ambapo tulikuwa watu kama sita au saba kwani walikuwepo Bozy, Orly, Nyomaa (Gaspar Karemera) na wanawake wawili akiwemo Zai ambaye alikuwa akituhudumia vinywaji. “Lakini Zai alijiunga nasi katika ile hali ya kawaida ya kampani na ilikuwa mara yetu ya kwanza kwenda naye club,” anasema Redondo.



ATUNZA FEDHA NA CHENI YA THAMANI



Wakiwa Maisha Club katika onyesho la Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia, Mafisango alikuwa akitunza fedha kila mara na waimbaji wakawa wanamuimba. Bozy ndiye aliyekuwa akitumwa fedha hizo kuzipeleka kwa waimbaji na ilifi ka wakati kabla hata ya kuwafi kia walikuwa wakianza kumuimba Mafisango.



Ndipo ulipofi ka muda alitoa cheni yake ya silva ili nayo ipelekwe kwa muimbaji mmoja, lakini Bozy akahoji vipi aitoe cheni hiyo? Lakini akaambiwa; “Peleka”. “Alinipa cheni yake ya silva ili nikamtunze muimbaji mmoja, ilikuwa ya gharama na nilipomuuliza akaniambia nimwambie muimbaji yule kwamba hiyo ni kumbukumbu yake kwani wanaweza wasionane tena.

“Tangu mchana alisema anataka kutumia fedha zote alizonazo siku hiyo hadi ziishe ndipo arejee nyumbani, na kweli hilo alilitekeleza,” anasema Bozy. Mafi sango alikuwa akigawa dola 100 (sasa ni zaidi ya Sh 220,000) kwa watu mbalimbali aliokutana nao na hata klabu alikuwa akitoa fedha hizo kwa waimbaji ambao walikuwa rafi ki zake.



REDONDO AONDOKA KLABU



Kabla ya saa 8:15 usiku, Redondo na rafi ki wengine wa Mafi sango waliondoka Maisha Club kwa kutumia usafi ri mwingine wa kukodi na kuwaacha wao watano yaani Mafi sango, Orly, Bozy, Nyomaa na yule dada Zai. Waliendelea na burudani huku wakinywa na kabla ya kuondoka, Orly na Bozy walikuwa hawaonekani ndipo Mafisango na yule dada wakatoka nje wakitaka kuondoka.



Baadaye akina Orly waliporudi walipoketi kina Mafi sango na kutowakuta, waliamua kwenda nje kuwafuata ndipo walipomkuta kiungo huyo wa zamani wa Simba akiwa amekasirika na kutaka funguo zake za gari huku akiwataka waondoke.



“Tangu asubuhi mimi ndiye niliyekuwa naendesha gari kwani Mafisango hakuwa mzoefu wa kuendesha gari Dar es Salaam hasa barabara kuu, nilisita kumpa funguo ili atuendeshe lakini sikuwa na jinsi. “Aliniambia yeye ndiye mwenye gari hivyo nimpe funguo, halafu kama kuna kitu kibaya anataka kimtokee yeye mwenyewe na siyo mtu mwingine pia alisema anataka aendeshe gari hilo mpaka mwisho wake.



“Hatukuelewa ana maana gani ila tuliona ni jambo la kawaida tu, nikampa funguo na safari ya kurejea nyumbani ikaanza,” anasema Bozy. Kabla ya kuelekea Chang’ombe walipitia Kinondoni kwanza kwa Redondo kumjulia hali kama amefi ka salama halafu wakaendelea na safari yao.



PALE KEKO KUMBE WALIGONGWA



Tofauti na ilivyoripotiwa awali kwamba Mafi sango alikuwa akiikwepa baiskeli ya matairi matatu maarufu kama Guta, ukweli ni kwamba waligongwa na gari lingine kwa nyuma.



Kama ilivyoelezwa awali kwamba, Mafi sango hakuwa na uzoefu sana barabarani hivyo baada ya kugongwa licha ya kuzidiwa na gari, asingeweza kuchukua hatua yoyote ile zaidi ya kuacha gari liende linavyotaka. “Ukweli kabla ya ajali ile kuna gari lilitugonga nyuma na dereva wa gari letu ambaye ni Mafi sango alipoteza uelekeo. “Baada ya kugongwa, Mafi sango alipoteza uelekeo na gari likaenda kugonga mti lakini kilikuwa ni kishindo kikubwa mno, gari lililotugonga halikuwa kubwa kama yale y a mizigo bali lilikuwa gari la saizi ya kati kama Nissan Patrol lakini lenye ngao kwa mbele.



“Baada ya kile kishindo mimi nilipoteza fahamu kwa muda kama wa dakika mbili hivi na nilipozinduka nikajikuta nipo nje ya gari chini ya mchanga, nikarudi katika gari na kumkuta Mafi sango ameumia akiwa ameinamia usukani,” anasema mmoja wa abiria waliokuwemo ndani ya gari hilo. Bozy aliyekuwa kwenye gari hilo wakati wa ajali, naye alithibitisha maneno ya abiria mwenzake kwa kusema: “Ni kweli tuligongwa kwa nyuma na gari lililotugonga lilikimbia.


“Ninachokumbuka ni kwamba Mafisango alikuwa akiendesha kwa mwendo wa spidi kati ya 80 hadi 100 na hakuwa mzuri sana barabarani, lakini licha ya kutokuwa na uzoefu na barabara za Dar es Salaam, huku mwanzo hakuweza kusababisha ajali hadi tulipofi ka Keko na kugongwa. “Lakini inauma sana kwani sielewi Mafi sango alikufaje kwani wote hatukuwa tumefunga mikanda ya usalama,” anasema Bozy.



Abiria wote yaani Zai, Nyomaa, Orly na Bozy hawakuumia sana na wala hawakutibiwa kwa muda mrefu, lakini Mafi sango alionekana kuumia sana kichwani katika paji na jichoni. Ikumbukwe kuwa Bozy si aliyetoa maelezo Polisi bali ni Orly na Nyomaa ndio waliofanya hivyo.



Hakika hizo ndizo saa 24 za mwisho za Mafisango!
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts