ALICHOKISEAMA KAMANDA SIRRO JUU YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA WALIOLALA SELO | BONGOJAMII

ALICHOKISEAMA KAMANDA SIRRO JUU YA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA WALIOLALA SELO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam limesema siyo lazima kila mtu aliyemo kwenye orodha ya Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda anayefika Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa alale mahabusu.



Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema wanalazimika kuwashikilia watu wenye viashiria ili kutafuta ukweli wa kuthibitisha yale yaliyofikiriwa kuona kama wanaweza kubaini lolote.


Siro amesema juzi walikwenda watu wa mahotelini (wamiliki), lakini baada ya kuhojiwa walionekana hawana jambo zito na la msingi, hivyo waliachiwa huru.


Kamanda huyo amesema kuna watu waliotajwa wanapiga simu kuulizia kuna nini na wengine wanawatuma ndugu zao.


“Hakuna sababu ya kuwa na woga mpaka kumtuma ndugu kwa Kamishna Siro, bali unapoitwa njoo uripoti kwa timu iliyoundwa na mkuu wa mkoa, watapeleleza mambo yote ukionekana huhusiki utaachiwa,” amesema.


“Kwa wale ambao hawajaripoti, ikifika kesho hawajafika hakuna shida, kikubwa ni kututaarifu juu ya udhuru wake. Unaweza ukasema mtu aje kumbe siku hiyo yupo kitandani, hakuna shida kwa kuwa lengo la upelelezi huu si kukomoa watu, bali ni kupata ukweli kuhusu hao watu.”


Pia, Siro amezungumzia kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema, “Kama Mbowe hawezi kuja sisi tutamfuata, wala hakuna shida katika hilo kwa sababu kama umeitwa na wewe hutaki kuja na sisi tunataka kukuhoji kujua ukweli kuhusiana na wewe, tutamfuata tu.”


Kamanda huyo amesema operesheni ya dawa ya kulevya bado inaendelea ambapo Jumatano walikamatwa watu 11 na kete 38 za dawa ya kulevya na magunia sita ya bangi.


“Waliokwishakamatwa wanaweza wakafikishwa mahakamani au wasifikishwe na kwamba utaratibu unaotumika sasa wa kuwatangaza watuhumiwa badala ya kuwakamata kuwafisha kituoni unawapa raha sana na unawarahisishia kazi polisi,” amesema.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts