DIAMOND PLATNUM AWASHANGAZA MASHABIKI ZAKE BAADA YA KUSHINDWA KUREJEA NA ZARI BONGO | BONGOJAMII

DIAMOND PLATNUM AWASHANGAZA MASHABIKI ZAKE BAADA YA KUSHINDWA KUREJEA NA ZARI BONGO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD



Msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaduwaza ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea baada ya kutua kutokea Sauzi akiwa peke yake, tofauti na ilivyotarajiwa kuwa angerejea na mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’.


Awali zilivuja taarifa kuwa, Diamond amekwenda Sauzi kumchukua Zari na mtoto wao aliyezaliwa hivi karibuni, Nillan ili waje kufanya sherehe kidogo.


Kufuatia taarifa hizo, Jumatatu iliyopita, nyakati za jioni, watu wa karibu na Diamond walifika ‘airport’ kuwapokea lakini kilichowashangaza wengi ni kumuona anatoka mwenyewe na mabegi yake, jambo lililowafanya wahisi kuna kitu.


“Hee, mbona yuko peke yake sasa? Zari na watoto wako wapi sasa? Au wamezinguana?” alisikika akisema mmoja wa akinadada waliokuwa uwanjani hapo.


Mbali na dada huyo, wengi walionekana kunong’ona kuonesha kutoamini wanachokiona na kwa kuwa Diamond alijua kuwa kawaangusha kwa kutokuja na Zari, hakuwa na mbwembwe zaidi ya kwenda kwenye gari lililokuwa limeletwa na kijana aitwaye Q Boy, wakaondoka zao.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts