HATIMAYE MNYIKA AANZA KUITIKISA SERIKALI UPYA BUNGENI KUPITIA JAMBO HILI ZITO | BONGOJAMII

HATIMAYE MNYIKA AANZA KUITIKISA SERIKALI UPYA BUNGENI KUPITIA JAMBO HILI ZITO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


MBUNGE wa Kibamba (Chadema), John Mnyika, ameiomba serikali kuhakikisha inawalipa fidia wakazi wa Mloganzila ambao waliacha maeneo yao na kupisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili (Muhas).


Akiuliza swali kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mnyika alisema baadhi ya wakazi wa eneo hilo walilipwa lakini miongoni mwao walipata kiasi ambacho hakilingani na maeneo yao, hivyo kuonekana kupunjwa.


Aidha, Mnyika alitaka kufahamu kwa jinsi gani serikali inashughulikia madai ya mapunjo ya fidia ya maendelezo kwa wakazi hao waliotakiwa kuondoka kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Muhas.


Hata hivyo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Angelina Mabula, alisema ahadi ya kuwalipa fidia ya kihisani yaani mkono wa heri iliyotolewa na serikali Mei 20, mwaka juzi, itafanyika baada ya kupatikana fedha.


Mabula alisema malipo hayo hayajafanyika kwa muda kutokana na ukosefu wa fedha kwenye bajeti, lakini pale zitakapopatikana hakuna atakayeshindwa kulipwa.


Alisema tayari serikali ilishalipa Sh. 8,067,904,700 kwa ajili ya fidia ya maendelezo ya ardhi kwa wananchi 1,919 katika kipindi cha 2008 mpaka 2010.


Aidha, alisema 2011 serikali ilitenga Sh. 1,610,374,700 kwa ajili ya fidia ya wananchi 619 waliosalia katika malipo hayo ya fidia, wakiwa wamewekeza ndani ya shamba mali ya serikali.


Hata hivyo, Mabula alisema mpaka sasa serikali haidaiwi mapunjo ya fidia kwa kuwa fidia ilikwishalipwa kwa mujibu wa sheria.A
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts