Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
ISHU hot iliyotrendi wiki hii ni kuhusu kigogo mmoja kudaiwa kumpangishia Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ mjengo wa maana uliopo Makongo Juu jijini Dar ambapo Ijumaa limechimba ili kujua ukweli wa mambo.
Madai hayo yaliibuka juzikati baada ya watu kibao wakiwemo mastaa kuhoji kwa nini modo huyo hakutajwa kwenye listi ya mastaa wa unga wakati aliwahi kunaswa akisafirisha ‘mzigo’ nchini Afrika Kusini na sasa anaishi maisha bomba.
“Unajua kati ya mastaa wanaoishi kwenye nyumba za kifahari Masogange yumo, watu wanasema anauza madawa lakini ninachojua mimi ni kwamba kapangishiwa bonge la jumba kule Makongo juu, ukifika pale utadhani anaishi bosi f’lani.
“Kapangishiwa na kigogo mmoja na huyo ndiye anampa jeuri mjini, sasa jaribuni kufuatilia mtaujua ukweli ila mimi msinitaje, msije mkanitafutia matatizo,” alidai mtoa ubuyu huyo.
Kufuatia madai hayo, Ijumaa lilifanya jitihada za kufahamu ilipo nyumba hiyo ambapo, kwa kuwatumia watu wanaomjua vizuri lilifanikiwa kufika Makongo Juu na kushuhudia nyumba hiyo ya kihafari.
Katika ‘kunyapianyapia’ ili kujua kama staa huyo alikuwemo ndani, paparazi wetu aligonga geti muda mrefu lakini halikuweza kufunguliwa wala kuonekana mtu yeyote.
Ijumaa laamua kumpigia simu
Waandishi wetu wakiwa wamekaa nje ya nyumba hiyo huku wakiangaza huku na kule, waliamua kumpigia simu Masogange na bahati nzuri alipokea na alipoambiwa wako nje kwake, alijibu kuwa hakuwepo hapo nyumbani.
“Sipo, niko mbali kidogo,” alisema mdada huyo mwenye figa matata.
Alipotakiwa kufungukia madai kuwa, nyumba hiyo anayoishi amepangiwa na kigogo mmoja maarufu na ndiye anayempa ujanja wa kuishi mjini, Masogange alisema kuwa ni kweli amepangiwa nyumba hiyo lakini siyo na kigogo kama inavyodaiwa.
“Watu wanasema eti nimepangiwa nyumba na kigogo, ukweli naujua mwenyewe. Nina mpenzi wangu na ndiye aliyenipangishia nyumba hii na hili suala lipo wazi kabisa kwani watu wangu wa karibu wanamjua,” alisema Masogange.
Aidha, katika muendelezo wa madai ya Masogange kupangiwa mjengo na kigogo, juzikati ilivuja clipu iliyodaiwa ni ya staa Wema Sepetu akihoji sababu za Masogange kutotajwa kwenye listi ya mastaa wa unga.
Hata hivyo, juzi kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na waandishi wa habari, mmoja wa mapaparazi alimuuliza sababu za Masogange kutotajwa kwenye listi hiyo kama alivyodaiwa kuhoji Wema ambapo mheshimiwa huyo aliyedhamiria kupambana vilivyo na biashara ya madawa ya kulevya katika Jiji la Dar alijibu:
“Kwanza ni kosa kisheria mtu anapokuwa anashikiliwa na jeshi la polisi kushika simu, sasa kama una jambo unataka kulisema na uko polisi, kwa nini usiliseme badala yake u.”
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka