SIMBA YAKILI KUDAIWA NA TRA, YAJIPANGA KULIPA DENI LAO | BONGOJAMII

SIMBA YAKILI KUDAIWA NA TRA, YAJIPANGA KULIPA DENI LAO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


Hatimaye Klabu ya Simba SC yajitokeza hadharani na kukiri kudaiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kodi za nyasi bandia walizozitelekeza bandarini huku wakifurahia kuongezewa muda wa kulipa malipo hayo.


Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni ya udalali ya MAJEMBE AUCTION kutangaza kuzipiga mnada endapo klabu hiyo itashindwa kwenda kulipia ushuru unaodaiwa.


"Simba inakiri kudaiwa na TRA kodi ya nyasi bandia, tunafanya juhudi zote kulipa kodi kwa wakati baada ya kuomba kuongezewa muda kulipa na TRA". Imeandika klabu hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii ya twiiter pamoja na instagram asubuhi ya leo (Ijumaa).


Pamoja na hayo klabu hiyo imewataka mashabiki na wanachama wake kuendelea kuwapa ushirikiano katika mechi zao za kanda ya ziwa vile vile kupuuza maneno ya mitandaoni yanayoweza kuwa na lengo baya kwa Simba SC.


Huu ndiyo ujumbe wao



Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts