WATAKAOCHINJA NG'OMBE KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA INDIA | BONGOJAMII

WATAKAOCHINJA NG'OMBE KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA INDIA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Ng'ome hutajwa kuwa mtakatifu na waumini wengi wa Hindu

Jimbo lililo magharibi mwa India la Gujarat, limepitisha sheria ya kuharamisha kuchinjwa ng'ome na kutangaza adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa yoyote ambaye atapatikana na kosa hilo.

Chini ya sheria hiyo, pia wale ambao watapatikana wakisafirisha nyama ya ng'ome watahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.

Ng'ome hutajwa kuwa mtakatifu na waumini wengi wa Hindu, na kumua ngome ni kitendo haramu katika majimbo mengi nchini India.

Kufuatia sheria hiyo jimbo la Gujarat sasa litakuwa na sheria kali zaidi kuhusu suala hilo nchini India.

Watakaopatikana na hatia watapigwa faini kali na kifungo gerezani. Faini ya kosa hilo imeongezwa kutoka dola 771 hadi dola 1542.

Waziri mmoja katika jimbo la Gujarat, aliawaambia waandishi wa habari kuwa ng'ome ni ishara ya utamaduni wa India

Sheria hizo mpya zitaanza kutekelezwa siku ya Jumamosi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts