Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-D2ANHKLo38TES9aWTH4IhuBvX5qdTytojLLczRw1fYPEwMLUOXPrTZjzDyzEbQx4EEajBEXgCdkg-iWeBnGWFybfJw4RI7vaMjDa6i056_fJr2KF7GaS1gFaiR1Ob8qyoyLONjuC2PrF/s640/handcuffed-620x350-750x375.jpg)
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ernest Makale, amesema mtuhumiwa huyo maarufu kama Simon Chomba ni mara yake ya tatu kukamatwa na maafisa wa TAKUKURU kwa kosa la kuwatapeli watu 13 aliokuwa akiwahaidi ajira ndani ya taasisi hiyo pamoja na kujifanya mtumishi wa TAKUKURU, jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 36 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Mbali na matukio ya kuchukua fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 4 laki mbili na themanini na nne elfu kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu,makale amesema chomba pia amekuwa akitumia cheo hicho cha Mkurugenzi wa TAKUKURU mkoa kujipatia huduma ya bure zikiwemo za kunyoa kwenye saloon, kitoweo cha samaki kutoka kwa wafanyabiashara na sehemu nyingine nyingi zinazotoa huduma kwa jamii.
Mtuhumiwa alikamatwa aprili 8 mwaka huu na maafisa wa TAKUKURU baada ya kuomba pesa kutoka kwa wananchi wawili kiasi cha jumla ya shilingi laki saba na elfu thelathini ili aweze kuwapatia kazi akijifanya kuwa ni Mkurugenzi wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza, ambapo mtego uliandaliwa mtego wa shilingi 100,000 ambao ndio ulifanikisha kukamatwa kwake.
Mtuhumiwa amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi na kupewa kesi namba 75 ya mwaka 2017 iliyopo mbele ya Hakimu Chuma. Mshitakiwa amesomewa mashitaka 13 na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Meela Mwema, hata hivyo amekosa dhamana na amerudishwa rumande hadi Aprili 19 mwaka huu kesi hiyo itapotajwa tena.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka