DK MZINDAKAYA AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO, ASEMA YUKO FITI NA ANA NGUVU ZAKUTOSHA | BONGOJAMII

DK MZINDAKAYA AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO, ASEMA YUKO FITI NA ANA NGUVU ZAKUTOSHA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Dk Chris Mzindakaya 

Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Dk Chris Mzindakaya amesikitishwa na watu wanaovumisha taarifa kuwa amefariki na kuwaita ni wapumbavu.

Akizungumza leo akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Mzindakaya amesema afya imeimarika zaidi na ataruhusiwa kuondoka hospitalini hapo wakati wowote. 

Usiku wa kuamkia leo mtandao ya kijamii ilikuwa ikisambaza taarifa potofu za kifo chake.

Baada ya uvumi huo,Dk Mzindakaya alitoa kauli hiyo leo huku akiwahakikishia waandishi kuwa baada ya matibabu, madaktari wamemweleza Afya yake imeimarika mfano wa kijana wa miaka 20.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts