HARMORAPA AFUNGUKA ADAI ANATAMANI KUFANYA COLLABO NA MSANII HUYU | BONGOJAMII

HARMORAPA AFUNGUKA ADAI ANATAMANI KUFANYA COLLABO NA MSANII HUYU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Harmorapa ni kati ya watu walioongelewa sana huu mwaka kwenye himaya tofauti tofauti hususan mitandaoni.

Rapper huyo ametusua kuhakikisha jina lake linatajwa midomoni mwa kila mtu kwenye kufanya muziki na matukio ya kusisimua na kuchekesha mno. Hiyo ndio sanaa halisi haswa. Nilipata nafasi ya kuzungumza naye masuala kuhusu muziki na issue nyingine.

Kati ya maswali niliyomuliza ni pamoja msanii gani anayemkubali nje ya Tanzania, hususan katika nchi za Afrika Mashariki. Jibu lake alimtaja rapper wa Kenya Prezzo. Alianza kwa kusimulia jinsi anavyomkubali jamaa.

“Prezzo namkubali sana toka kitambo, tokea niko chini shule ya msingi. Nilikuwa namkubali sana swagga zake na rap zake zilikuwa zinanifurahisha sana na zinanifurahisha mpaka kesho kiukweli.”

Hakijatosha, rapper huyo machachari aliendelea kusema, “So kwahiyo natamani sana one day nifanye naye collabo kwahiyo kama nikipata nafasi kufanya naye itakuwa very good nitashukuru Mungu,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Harmorapa amesema ana kazi zingine zipo jikoni mapishi yanaendelea. Amemtaka kila mmoja kuwa tayari kwakuwa wimbo wake Kiboko ya Mabishoo umempa nguvu za kufanya makubwa.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts