HIKI NDICHO KILICHO WAKUTANISHA NUHU NA SHILOLE ZANZIBAR | BONGOJAMII

HIKI NDICHO KILICHO WAKUTANISHA NUHU NA SHILOLE ZANZIBAR

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii wa bongo fleva Nuh Mziwanda amesema Shilole ni msanii mwenzake na walivyoenda Zanzibar hawakuwa pamoja kila mtu alikuwa ameenda kwa kazi yake.

Akipiga story kupitia eNewz ya EATV Nuh Mziwanda amesema hata kama akiamua kutoka nje ya ndoa siyo lazima atoke na Shilole kwakuwa wanawake ni wengi na anapokuwa kwenye show huwa anakutana na wanawake wengi hivyo siyo lazima atembee na Shilole..

Hata hivyo Nuh Mziwanda amesema haoni sababu ya kutoka nje ya ndoa yake na mashabiki zake wanapaswa kuelewa kwamba anapokuwa kwenye show moja na Shilole ni kutokana na maslahi hawezi kukataa pesa eti kwa sababu show aliyopata Shilole yupo.

Pia Nuh alimalizia kwa kusema "Zanzibar kila mtu alienda kwa kazi zake japo tulijikuta tumeshukia hotel moja, Shilole akiwa ameenda kuzindua Pub lakini mimi nilikuwa nimeitwa na nimepewa pesa zangu kwa ajili ya kufanya show"
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts