WEMA SEPETU AFUNGUKA MAZITO JUU YA HARMORAPA | BONGOJAMII

WEMA SEPETU AFUNGUKA MAZITO JUU YA HARMORAPA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
DAR ES SALAAM: Acha hizo! Vituko vya Mbongo Fleva anayekuja kwa kasi nchini, Athumani Omar ’Harmorapa’ haviishi, juzikati tena, ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akionesha hisia za mapenzi kwa Miss Tanzania 2006 aliye pia staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu huku Wema sasa akimbeza msanii huyo.
Harmorapa aliandika anavyomzimikia nyota huyo, akaanika urefu wa muda ambao alianza kumpenda kwamba ni kipindi anaingia kwenye ulimbwende na kutwaa taji.

Harmorapa alikwenda mbele zaidi kwa kutoboa siri hata alivyokosa raha pale, Wema alipokatwa jina kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, uchaguzi wa mwaka 2015.

Mwishowe, Harmorapa alisema yu tayari kuwa na Wema kimapenzi na ikitokea, atamvisha pete ya uchumba na kuwa wake sanjari na kumtunza kama wake. Soma hii:

“Napenda kusema ukweli ulio moyoni mwangu tangu siku nyingi ninavyosumbuliwa na hisia za kimapenzi kwa Wema Sepetu, tangu naanza kumfahamu na kumwona kwenye tv akigombea u-miss TZ, mwaka 2006, nilitokea kumpenda sana na kupata hisia za kumuoa, basi tu ndo’ vile nilikuwa sina uwezo wa kuonana naye wala kukutana naye kwa sababu ya nafasi niliyokuwa nayo enzi hizo nauza mapochi Mwenge.

“Nakumbuka kipindi kile, Wema wamemkata kwenye uchaguzi wa wabunge wa viti maalum niliumia hadi sikupata usingizi. Niliamka saa 9 usiku gheto na kuelekea Mwenge kuchukua mikoba ya kuiuza. Rafi ki yangu alinipa taarifa kuwa, Wema anaingia Dar kutokea Dodoma.

“Nilisema lazima nikampokee na zawadi nimpe, basi kwenye mikoba kule nilibahatika kupata mmoja mzuri sana, akili ikanijia kuwa ule nimpe zawadi Wema.

“Baadaye nikafunga goli ‘duka la biashara’ mapema, nikaenda kumpokea. Baada ya madam kufi ka nilihangaika sana ili nimfi kie nimpe zawadi ya mkoba, bahati mbaya niligongwa na bodaboda mguu wa kushoto na sikufanikiwa kumpa ila hadi leo mkoba ninao.

“Naombeni mumfi kishie taarifa hizi Wema, mwambieni nampenda sana endapo nitampata hatochukua hata wiki kwangu, n’tamvisha pete na kufunga naye ndoa na kumtunza kwa hali yoyote ile.”

Baada ya ujumbe huo, Uwazi lilimtafuta Wema na kumsomea mwanzo hadi mwisho, akasema: “Jamani! Harmorapa! Ila sasa hapo kwenye pete ya uchumba na kunitunza sina hakika miye.”

Wema alipoulizwa kwa nini hana hakika na eneo hilo tu, alishindwa kufafanua hali iliyotafsirika kuwa, maeneo mengine alikubaliana na msanii huyo kasoro kwenye umalizikiaji wake kwamba, Harmorapa hawezi kumvisha pete wala kumtunza yeye, pengine kwa kipato au ubahili wa msanii huyo kama amewahi kuusikia.


Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts