HIKI NDICHO KIWANGO CHA MISHAHARA SHILOLE ANACHOWALIPA WAFANYAKAZI WAKE | BONGOJAMII

HIKI NDICHO KIWANGO CHA MISHAHARA SHILOLE ANACHOWALIPA WAFANYAKAZI WAKE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Moja kati ya stori kubwa mitandaoni ni kuhusu staa wa Bongofleva Shilole kugeukia katika ujasiliamali mbali na muziki ambapo amefungua mgahawa unaoitwa Shishi Trump kwa lengo la kujiongezea kipato.

Usiku wa April 14 2017 kupitia The Weekend Chart Show ya Clouds TV, Shilole alizungumzia maendeleo ya biashara yake hiyo akiweka wazi kiwango cha mshahara anachowalipa wafanyakazi wake 10 waliopo mgahawani kuwa ni Shilingi 200,000 kila mmoja lakini mtu wa jikoni analipwa zaidi.

>>>”Nimeajiri watu kumi na kila mfanyakazi wangu hapa analipwa Laki Mbili japo inategemea. Mfanyakazi wa jikoni ndio analipwa hela nyingi, ila mimi sijilipi. Nawa-manage vizuri maana tunapata wateja wengi na wafanyakazi wanajituma. Kuna mtu kama Pendo ambaye nimetoka naye mbali, so, anafanya kazi vizuri. Ananifurahisha.” – Shilole

Katika hatua nyingine Shilole alielezea tukio la kuvunjwa kwenye eneo la biashara yake na watu wasiofahamika kisha kuiba TV, Radio, vinywaji na baadhi ya vitu:>>>”Alikuja meneja wangu kashika mikono kichwani, akanieleza kuwa tumeibiwa, vinywaji vimechukuliwa vyote. Ikabidi nije naye ofisini na kukuta watu wameiba TV, Radio na vinywaji. Nilipata hasara ila sikufunga biashara. Jioni nilienda kununua vinywaji na biashara ikaendelea.” – Shilole.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts