HUU NDIO MJI UNAOJENGWA SAUDIA ARABIA MAALUM KWA BURUDANI TU | BONGOJAMII

HUU NDIO MJI UNAOJENGWA SAUDIA ARABIA MAALUM KWA BURUDANI TU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Saudi Arabia imeanzisha mipango ya kujenga mji wa burudani kando mwa mji wa Riyadh ambao utakuwa mkubwa mara 50 zaidi ya himaya ya Uingereza ya Gibraltar.


Mji huo ambao utakuwa na ukubwa wa kilomita 334 mraba ambao utakuwa sawa na mji wa Las Vegas, utatoa huduma za kitamaduni, michezo na mambo mengine ya burudani.


Inaripotiwa kuwa mji utakuwa wa aina yake duniani.


Ujenzi wa mji huo utataanza mapema mwaka ujao na awamu ya kwanza kukamilika mwaka 2022.


Katika malengo ya mwaka 2030 uliotangazwa na naibu mfalme Mohammad Bin Salman mwaka mmoja ulipita, una lengo la kuboresha uchumi na kuzuia kutegemea mafuta kwa taifa hilo.


Mji huo ambao ni kama sehemu moja ya tano ya mji wa Riyadh, ndio mradi wa hivi punde kutangazwa.


Utawala unasema kuwa matumaini ni kuwa utawavutia wageni, kuboresha uchumi na ukawa wa burudani na furara kwa wale wataishi mji mkuu Riyadh.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts