TAHADHARI YATOLEWA JUU YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA TANZANIA | BONGOJAMII

TAHADHARI YATOLEWA JUU YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA TANZANIA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa Watanzania juu ya kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia leo Jumatatu hadi Jumatano.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoitoa leo (Jumatatu), mamlaka hiyo imesema kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.


Mamlaka hiyo imesema mikoa itakayoathirika ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.


“Mvua hii yenye wastani wa asilimia 60, inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini,” imesema taarifa hiyo.


Kutokana na hali hiyo, mamlaka imewataka wakazi mikoa hiyo kuchukua hatua stahiki.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts