VIDEO: WAKUU WA MIKOA , WABUNGE, WAKUU WA WILAYA.WASALIMIKA SAKATA LA VYETI FEKI | BONGOJAMII

VIDEO: WAKUU WA MIKOA , WABUNGE, WAKUU WA WILAYA.WASALIMIKA SAKATA LA VYETI FEKI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
DODOMA: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki leo Aprili 28, 2017 amekabidhi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti vya Watumishi wa Umma.


Akikabidhi taarifa hiyo kwa Rais Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Rais amesema kuwa, Wizara yake iliagiza NECTA kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vya uwalimu.


“Jumla ya watumishi wa umma 435,000 wamefanyiwa uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma, Watumishi 9932 kati ya watumishi waliohakikiwa walikutwa na vyeti vya kughushi, Vyeti vyenye utata. Vyeti 1538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya watu 3076”


“Uhakiki huu haujafanyika kwa viongozi wa kisiasa kwa sababu wao wanahitajika kujua kusoma na kuandika tu.


“Pia Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wabunge na Madiwani hawajahakikiwa vyeti vyao vya taaluma kwa kuwa mamlaka ya uteuzi ndiyo wanajua ufanisi wa kazi zao.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts