YERIKO NYERERE APANDISHA MAHAKAMANI KISUTU | BONGOJAMII

YERIKO NYERERE APANDISHA MAHAKAMANI KISUTU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mfanyabiashara na kada maarufu wa CHADEMA Yericko Nyerere amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano ya kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa Facebook.

Kwa mujibu wa kesi hiyo namba 184, 2017, Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Wilbard Mashauri kuwa mshtakiwa huyo alifanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao Namba 14 ya 2015

Ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye amesaini bondi ya Sh 10milioni.

Kesi imeahirishwa Juni 5, 2017 kusomewa maelezo ya awali (PH)

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts